Families and elders pray from Jerusalem's wall as countless hostile tents and banners fill the valley

Zaburi 83

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
1Ee Mungu, usikae kimya, usinyamaze, Ee Mungu, usikae mbali.
2Tazama watesi wako wanafanya fujo, jinsi adui zako wanavyoinua vichwa vyao.
3Kwa ujanja, wanapanga njama dhidi ya watu wako; wanapanga hila dhidi ya wale unaowapenda.
4Wanasema, “Njooni, tuwaangamize kama taifa, ili jina la Israeli lisikumbukwe tena.”
5Kwa nia moja wanapanga njama pamoja, wanafanya muungano dhidi yako,
6mahema ya Edomu na Waishmaeli, ya Wamoabu na Wahagari,
7Gebali , Amoni na Amaleki, Ufilisti, pamoja na watu wa Tiro.
8Hata Ashuru wameungana nao kuwapa nguvu wazao wa Lutu.
9Uwatendee kama vile ulivyowatendea Midiani, na kama vile ulivyowatendea Sisera na Yabini hapo kijito cha Kishoni,
10ambao waliangamia huko Endori na wakawa kama kinyesi juu ya ardhi.
11Wafanye wakuu wao kama Orebu na Zeebu, watawala wao kama Zeba na Salmuna,
12ambao walisema, “Na tumiliki maeneo ya malisho ya Mungu.”
13Ee Mungu wangu, wapeperushe kama mavumbi ya kisulisuli, kama makapi yapeperushwayo na upepo.
14Kama vile moto unavyoteketeza msitu au mwali wa moto unavyounguza milima,
15wafuatilie kwa tufani yako na kuwafadhaisha kwa dhoruba yako.
16Funika nyuso zao kwa aibu ili watu walitafute jina lako, Ee Mwenyezi Mungu.
17Wao na waaibishwe na kufadhaishwa milele, na waangamie kwa aibu.
18Hebu wajue kuwa wewe, ambaye jina lako ni Mwenyezi Mungu, kwamba wewe peke yako ndiwe Uliye Juu Sana ya dunia yote.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu — CC BY-SA 4.0. Where these translations come from.

Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc. Available free at biblica.com and open.bible. Text unchanged, used under CC BY-SA 4.0.