
Zaburi 82
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
1Mungu anaongoza kusanyiko kuu, anatoa hukumu miongoni mwa “miungu”:
2“Hata lini utaendelea kuwatetea wasio haki na kuonesha upendeleo kwa waovu?
3Teteeni wanyonge na yatima, tunzeni haki za maskini na waliodhulumiwa.
4Mwokoeni mnyonge na mhitaji, wakomboeni kutoka mkononi mwa mwovu.
5“Hawajui lolote, hawaelewi lolote. Wanatembea gizani; misingi yote ya dunia imetikisika.
6“Nilisema, ‘Ninyi ni “miungu”; ninyi nyote ni wana wa Aliye Juu Sana.’
7Lakini mtakufa kama wanadamu wa kawaida; mtaanguka kama mtawala mwingine yeyote.”
8Ee Mungu, inuka uihukumu nchi, kwa kuwa mataifa yote ni urithi wako.
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu — CC BY-SA 4.0. Where these translations come from.
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc. Available free at biblica.com and open.bible. Text unchanged, used under CC BY-SA 4.0.