
Zaburi 47
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
1Pigeni makofi, enyi mataifa yote, mpigieni Mungu kelele za shangwe!
2Jinsi gani alivyo wa kutisha, Mwenyezi Mungu Aliye Juu Sana, Mfalme mkuu juu ya dunia yote!
3Ametiisha mataifa chini yetu, watu wengi chini ya miguu yetu.
4Alituchagulia urithi wetu, fahari ya Yakobo, aliyempenda.
5Mungu amepaa kwa kelele za shangwe, Mwenyezi Mungu kwa sauti za tarumbeta.
6Mwimbieni Mungu sifa, imbeni sifa, mwimbieni sifa Mfalme wetu, imbeni sifa.
7Kwa kuwa Mungu ni mfalme wa dunia yote, mwimbieni zaburi za sifa.
8Mungu anayatawala mataifa, Mungu ameketi kwenye kiti chake cha enzi kitakatifu.
9Wakuu wa mataifa wanakusanyika kama watu wa Mungu wa Ibrahimu, kwa kuwa wafalme wa dunia ni mali ya Mungu; yeye ametukuka sana.
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu — CC BY-SA 4.0. Where these translations come from.
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc. Available free at biblica.com and open.bible. Text unchanged, used under CC BY-SA 4.0.