
Zaburi 20
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
1Mwenyezi Mungu na akujibu unapokuwa katika dhiki, jina la Mungu wa Yakobo na liwe kinga yako.
2Na akutumie msaada kutoka patakatifu na akupatie msaada kutoka Sayuni.
3Na azikumbuke dhabihu zako zote, na azikubali sadaka zako za kuteketezwa.
4Na akujalie haja ya moyo wako, na aifanikishe mipango yako yote.
5Tutashangilia kwa furaha utakaposhinda, tutainua bendera zetu kwa jina la Mungu wetu. Mwenyezi Mungu na akupe haja zako zote.
6Sasa nafahamu kuwa Mwenyezi Mungu humwokoa mpakwa mafuta wake, humjibu kutoka mbingu yake takatifu kwa nguvu za wokovu wa mkono wake wa kuume.
7Wengine wanatumaini magari ya vita, na wengine farasi, bali sisi tutalitumainia jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wetu.
8Wao wameshushwa chini na kuanguka, bali sisi tunainuka na kusimama imara.
9Ee Mwenyezi Mungu, mwokoe mfalme! Tujibu tunapokuita!
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu — CC BY-SA 4.0. Where these translations come from.
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc. Available free at biblica.com and open.bible. Text unchanged, used under CC BY-SA 4.0.