
Zaburi 150
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
1Msifuni Mwenyezi Mungu. Msifuni Mungu katika patakatifu pake, msifuni katika mbingu zake kuu.
2Msifuni kwa matendo yake makuu, msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.
3Msifuni kwa mvumo wa tarumbeta, msifuni kwa kinubi na zeze,
4msifuni kwa matari na kucheza, msifuni kwa kinanda cha nyuzi na filimbi,
5msifuni kwa matoazi yaliayo, msifuni kwa matoazi yavumayo sana.
6Kila chenye pumzi na kimsifu Mwenyezi Mungu. Msifuni Mwenyezi Mungu!
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu — CC BY-SA 4.0. Where these translations come from.
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc. Available free at biblica.com and open.bible. Text unchanged, used under CC BY-SA 4.0.