Musicians and dancers rejoice before elders as subdued rulers sit beside peacefully surrendered weapons

Zaburi 149

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
1Msifuni Mwenyezi Mungu. Mwimbieni Mwenyezi Mungu wimbo mpya, sifa zake katika kusanyiko la watakatifu.
2Israeli na washangilie katika Muumba wao, watu wa Sayuni na wafurahi katika Mfalme wao.
3Na walisifu jina lake kwa kucheza na wampigie muziki kwa matari na kinubi.
4Kwa maana Mwenyezi Mungu anapendezwa na watu wake, anawavika wanyenyekevu taji la wokovu.
5Watakatifu washangilie katika heshima hii, na waimbe kwa shangwe vitandani mwao.
6Sifa za Mungu na ziwe vinywani mwao na upanga ukatao kuwili mikononi mwao,
7ili walipize mataifa kisasi na adhabu juu ya mataifa,
8wawafunge wafalme wao kwa minyororo, wakuu wao kwa pingu za chuma,
9ili kuwafanyia hukumu iliyoandikwa dhidi yao. Huu ndio utukufu wa watakatifu wake wote. Msifuni Mwenyezi Mungu.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu — CC BY-SA 4.0. Where these translations come from.

Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc. Available free at biblica.com and open.bible. Text unchanged, used under CC BY-SA 4.0.