
Zaburi 145
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
1Nitakutukuza wewe, Mungu wangu Mfalme, nitalisifu jina lako milele na milele.
2Kila siku nitakusifu na kulitukuza jina lako milele na milele.
3Mwenyezi Mungu ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana, ukuu wake haupimiki.
4Kizazi kimoja kitasifia kazi zako kwa kizazi kingine, watasimulia matendo yako makuu.
5Watasema juu ya utukufu wa fahari ya ukuu wako, nami nitatafakari juu ya kazi zako za ajabu.
6Watasimulia uwezo wa kazi zako za kutisha, nami nitatangaza matendo yako makuu.
7Wataadhimisha wema wako mwingi, na wataimba kwa shangwe kuhusu haki yako.
8Mwenyezi Mungu ni mwenye neema na mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira, bali ni mwingi wa upendo.
9Mwenyezi Mungu ni mwema kwa wote, ana huruma kwa vyote alivyovifanya.
10Ee Mwenyezi Mungu, vyote ulivyovifanya vitakusifu, watakatifu wako watakutukuza.
11Watasimulia utukufu wa ufalme wako na kusema kuhusu ukuu wako,
12ili watu wote wajue matendo yako makuu na utukufu wa fahari ya ufalme wako.
13Ufalme wako ni ufalme wa milele, mamlaka yako hudumu vizazi vyote. Mwenyezi Mungu ni mwaminifu kwa ahadi zake zote na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya.
14Mwenyezi Mungu huwategemeza wote waangukao, na huwainua wote waliolemewa na mizigo yao.
15Macho ya watu wote yanakutazama, nawe huwapa chakula chao wakati wake.
16Waufumbua mkono wako, watosheleza haja ya kila kitu kilicho hai.
17Mwenyezi Mungu ni mwenye haki katika njia zake zote, na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya.
18Mwenyezi Mungu yu karibu na wote wamwitao, karibu na wote wamwitao kwa uaminifu.
19Huwatimizia wamchao matakwa yao, husikia kilio chao na kuwaokoa.
20Mwenyezi Mungu huwalinda wote wanaompenda, bali waovu wote atawaangamiza.
21Kinywa changu kitazinena sifa za Mwenyezi Mungu. Kila kiumbe na kilisifu jina lake takatifu milele na milele.
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu — CC BY-SA 4.0. Where these translations come from.
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc. Available free at biblica.com and open.bible. Text unchanged, used under CC BY-SA 4.0.