An elder shows healed scars to younger listeners beside cut ropes as former oppressors leave

Zaburi 129

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
1Wamenitesa sana tangu ujana wangu; Israeli na aseme sasa:
2wamenitesa sana tangu ujana wangu, lakini bado hawajanishinda.
3Wakulima wamelima mgongo wangu, na kufanya mifereji yao mirefu.
4Lakini Mwenyezi Mungu ni mwenye haki; amenifungua toka kamba za waovu.
5Wale wote wanaoichukia Sayuni na warudishwe nyuma kwa aibu.
6Wawe kama majani juu ya paa, ambayo hunyauka kabla hayajakua;
7kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake, wala akusanyaye kujaza mikono yake.
8Wale wapitao karibu na wasiseme, “Baraka ya Mwenyezi Mungu iwe juu yako; tunakubariki katika jina la Mwenyezi Mungu.”

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu — CC BY-SA 4.0. Where these translations come from.

Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc. Available free at biblica.com and open.bible. Text unchanged, used under CC BY-SA 4.0.