Three generations share a courtyard meal beneath grapes and olives overlooking peaceful Jerusalem

Zaburi 128

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
1Heri wale wote wamchao Mwenyezi Mungu, wanaoenda katika njia zake.
2Utakula matunda ya kazi yako; baraka na mafanikio vitakuwa vyako.
3Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao ndani ya nyumba yako; wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeituni kuizunguka meza yako.
4Hivyo ndivyo atakavyobarikiwa mtu amchaye Mwenyezi Mungu.
5Mwenyezi Mungu na akubariki kutoka Sayuni siku zote za maisha yako, na uone mafanikio ya Yerusalemu,
6nawe ujaliwe kuishi uone watoto wa watoto wako. Amani iwe juu ya Israeli.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu — CC BY-SA 4.0. Where these translations come from.

Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc. Available free at biblica.com and open.bible. Text unchanged, used under CC BY-SA 4.0.