A watchman guards families on a mountain road as night becomes dawn near distant Jerusalem

Zaburi 121

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
1Nayainua macho yangu natazama milima: msaada wangu utatoka wapi?
2Msaada wangu hutoka kwa Mwenyezi Mungu, Muumba wa mbingu na dunia.
3Hatauacha mguu wako uteleze, yeye akulindaye hatasinzia,
4hakika, yeye alindaye Israeli hatasinzia wala hatalala usingizi.
5Mwenyezi Mungu anakulinda, Mwenyezi Mungu ni uvuli wako mkono wako wa kuume,
6jua halitakudhuru mchana, wala mwezi wakati wa usiku.
7Mwenyezi Mungu atakukinga na madhara yote, atayalinda maisha yako,
8Mwenyezi Mungu atakulinda unapoingia na unapotoka, tangu sasa na hata milele.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu — CC BY-SA 4.0. Where these translations come from.

Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc. Available free at biblica.com and open.bible. Text unchanged, used under CC BY-SA 4.0.