
Zaburi 120
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
1Katika dhiki yangu namwita Mwenyezi Mungu, naye hunijibu.
2Ee Mwenyezi Mungu, uniokoe kutoka midomo ya uongo na ndimi za udanganyifu.
3Atakufanyia nini, au akufanyie nini zaidi, ewe ulimi mdanganyifu?
4Atakuadhibu kwa mishale mikali ya shujaa, kwa makaa yanayowaka ya mti wa mretemu.
5Ole wangu kwa kuwa naishi Mesheki, kwamba naishi katikati ya mahema ya Kedari!
6Nimeishi muda mrefu mno miongoni mwa wale wanaochukia amani.
7Mimi ni mtu wa amani; lakini ninaposema, wao wanataka vita.
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu — CC BY-SA 4.0. Where these translations come from.
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc. Available free at biblica.com and open.bible. Text unchanged, used under CC BY-SA 4.0.