Travelers support a wounded man along a rain-wet road toward dawn while an unused altar stands beneath fading mist

Hosea 6

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
1“Njooni, tumrudie Mwenyezi Mungu. Ameturarua vipande vipande lakini atatuponya; ametujeruhi lakini atatufunga majeraha yetu.
2Baada ya siku mbili atatufufua; katika siku ya tatu atatuinua, ili tuweze kuishi mbele zake.
3Tumkubali Mwenyezi Mungu, tukaze kumkubali yeye. Kutokea kwake ni hakika kama vile kuchomoza kwa jua; atatujia kama mvua za masika, kama vile mvua za vuli ziinyweshavyo nchi.”
4“Nifanye nini nawe, Efraimu? Nifanye nini nawe, Yuda? Upendo wako ni kama ukungu wa asubuhi, kama umande wa alfajiri utowekao.
5Kwa hiyo nimewakata ninyi vipande vipande nikitumia manabii wangu; nimewaua ninyi kwa maneno ya kinywa changu, hukumu zangu zinawaka kama umeme juu yenu.
6Kwa maana nataka rehema, wala si dhabihu, na kumkubali Mungu kuliko sadaka za kuteketezwa.
7Wamevunja agano kama Adamu: hawakuwa waaminifu kwangu huko.
8Gileadi ni mji wa watenda maovu, umetiwa madoa kwa nyayo za damu.
9Kama wanyang’anyi wamviziavyo mtu, ndivyo magenge ya makuhani wafanyavyo; wanaulia watu kwenye njia iendayo Shekemu, wakifanya uhalifu wa aibu.
10Nimeona jambo la kutisha katika nyumba ya Israeli. Huko Efraimu amejitolea kwa ukahaba na Israeli amenajisika.
11“Pia kwa ajili yako, Yuda, mavuno yameamriwa. “Wakati wowote ningerejesha neema ya watu wangu,

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu — CC BY-SA 4.0. Where these translations come from.

Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc. Available free at biblica.com and open.bible. Text unchanged, used under CC BY-SA 4.0.