
Zaburi 98
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
1Mwimbieni Mwenyezi Mungu wimbo mpya, kwa maana ametenda mambo ya ajabu; kitanga chake cha kuume na mkono wake mtakatifu umemfanyia wokovu.
2Mwenyezi Mungu ameufanya wokovu wake ujulikane na amedhihirisha haki yake kwa mataifa.
3Ameukumbuka upendo wake na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli; miisho yote ya dunia imeuona wokovu wa Mungu wetu.
4Mpigieni Mwenyezi Mungu kelele za shangwe, dunia yote, ipaze sauti kwa nyimbo za shangwe na vinanda;
5mwimbieni Mwenyezi Mungu kwa kinubi, kwa kinubi na sauti za kuimba,
6kwa tarumbeta na mvumo wa baragumu za pembe za kondoo dume: shangilieni kwa furaha mbele za Mwenyezi Mungu, aliye Mfalme.
7Bahari na ivume na kila kilicho ndani yake, dunia na wote wanaoishi ndani yake.
8Mito na ipige makofi, milima na iimbe pamoja kwa furaha,
9vyote na viimbe mbele za Mwenyezi Mungu, kwa maana yuaja kuhukumu dunia. Atahukumu dunia kwa haki na mataifa kwa haki.
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu — CC BY-SA 4.0. Where these translations come from.
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc. Available free at biblica.com and open.bible. Text unchanged, used under CC BY-SA 4.0.