Families from many lands gather with musicians and dancers inside Jerusalem's open gates

Zaburi 87

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
1Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu;
2Mwenyezi Mungu anayapenda malango ya Sayuni kuliko makao yote ya Yakobo.
3Mambo matukufu yanasemwa juu yako, ee mji wa Mungu:
4“Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu na Babeli miongoni mwa wale wanaonikubali mimi: Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi, nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ ”
5Kuhusu Sayuni itasemwa hivi, “Huyu na yule walizaliwa humo, naye Aliye Juu Sana mwenyewe atamwimarisha.”
6Mwenyezi Mungu ataandika katika orodha ya mataifa: “Huyu alizaliwa Sayuni.”
7Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba, “Chemchemi zangu zote ziko kwako.”

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu — CC BY-SA 4.0. Where these translations come from.

Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc. Available free at biblica.com and open.bible. Text unchanged, used under CC BY-SA 4.0.