
Zaburi 75
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
1Ee Mungu, tunakushukuru, tunakushukuru wewe, kwa kuwa jina lako li karibu; watu husimulia matendo yako ya ajabu.
2Unasema, “Ninachagua wakati maalum; ni mimi nihukumuye kwa haki.
3Dunia inapotetemeka na watu wake wote, ni mimi ninayezishikilia nguzo zake imara.
4Kwa wale wenye majivuno ninasema, ‘Msijisifu tena,’ kwa wale waovu, ‘Msiinue pembe zenu.
5Msiinue pembe zenu dhidi ya mbingu; msiseme kwa kiburi.’ ”
6Hakuna yeyote atokaye mashariki wala magharibi au kutoka jangwani awezaye kumkweza mwanadamu.
7Bali Mungu ndiye ahukumuye: Humshusha huyu na kumkweza mwingine.
8Mkononi mwa Mwenyezi Mungu kuna kikombe kilichojaa mvinyo unaotoka povu uliochanganywa na vikolezo; huumimina, nao waovu wote wa dunia hunywa hata tone la mwisho.
9Bali mimi, nitatangaza hili milele; nitaimba sifa kwa Mungu wa Yakobo.
10Nitazikatilia mbali pembe za waovu wote, bali pembe za wenye haki zitainuliwa juu.
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu — CC BY-SA 4.0. Where these translations come from.
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc. Available free at biblica.com and open.bible. Text unchanged, used under CC BY-SA 4.0.