
Zaburi 70
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
1Ee Mungu, ufanye haraka kuniokoa; Ee Mwenyezi Mungu, njoo hima unisaidie.
2Wale wanaotafuta kuniua, waaibishwe na kufadhaishwa; wote wanaotamani kuangamizwa kwangu, warudishwe nyuma kwa aibu.
3Wale wanaoniambia, “Aha! Aha!” na warudi nyuma kwa sababu ya aibu yao.
4Lakini wote wanaokutafuta washangilie na kukufurahia, wale wanaoupenda wokovu wako siku zote waseme, “Mwenyezi Mungu ni mkuu!”
5Lakini mimi bado ni maskini na mhitaji; Ee Mungu, unijie haraka. Wewe ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu; Ee Mwenyezi Mungu, usikawie.
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu — CC BY-SA 4.0. Where these translations come from.
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc. Available free at biblica.com and open.bible. Text unchanged, used under CC BY-SA 4.0.