A sick man prays from bed while companions wait and sunrise enters the room

Zaburi 6

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
1Ee Mwenyezi Mungu, usinikemee katika hasira yako, wala usiniadhibu katika ghadhabu yako.
2Unirehemu Mwenyezi Mungu, kwa maana nimedhoofika; Ee Mwenyezi Mungu, uniponye, kwa maana mifupa yangu ina maumivu makali.
3Nafsi yangu ina uchungu mwingi. Hadi lini, Ee Mwenyezi Mungu, hadi lini?
4Geuka, Ee Mwenyezi Mungu, unikomboe, uniokoe kwa sababu ya fadhili zako.
5Hakuna mtu anayekukumbuka akiwa amekufa. Ni nani awezaye kukusifu akiwa Kuzimu ?
6Nimechakaa kwa kulia kwa huzuni; usiku kucha natiririsha kitanda changu kwa machozi; nimelowesha kiti changu kwa machozi yangu.
7Macho yangu yamedhoofika kwa kuhuzunika, yamedhoofika kwa sababu ya adui zangu wote.
8Kaeni mbali nami, ninyi nyote mtendao mabaya, kwa maana Mwenyezi Mungu amesikia kulia kwangu.
9Mwenyezi Mungu amesikia kilio changu kwa huruma, Mwenyezi Mungu amekubali sala yangu.
10Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika, watarudi nyuma na waaibishwe kwa ghafula.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu — CC BY-SA 4.0. Where these translations come from.

Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc. Available free at biblica.com and open.bible. Text unchanged, used under CC BY-SA 4.0.