A watched captive holds a tear bottle before walking toward dawn past broken chains

Zaburi 56

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
1Ee Mungu unihurumie, maana watu wananifuatia vikali; mchana kutwa wanazidisha mashambulizi yao.
2Wasingiziaji wangu wananifuatia mchana kutwa, wengi wananishambulia kwa kiburi chao.
3Wakati ninaogopa, nitakutumaini wewe.
4Katika Mungu, ambaye neno lake ninalisifu, katika Mungu ninatumaini, sitaogopa. Mwanadamu mwenye kufa atanitenda nini?
5Mchana kutwa wanayageuza maneno yangu, siku zote wanapanga njama za kunidhuru.
6Wananifanyia hila, wanajificha, wanatazama hatua zangu, wakiwa na shauku ya kuutoa uhai wangu.
7Wasiepuke kwa vyovyote, Ee Mungu, katika hasira yako yaangushe mataifa.
8Andika maombolezo yangu; andika machozi yangu katika kitabu chako: je, haya hayapo katika kumbukumbu zako?
9Ndipo adui zangu watarudi nyuma ninapoita msaada. Kwa hili nitajua kwamba Mungu yuko upande wangu.
10Katika Mungu, ambaye neno lake ninalisifu, katika Mwenyezi Mungu, ambaye neno lake ninalisifu,
11katika Mungu ninatumaini, sitaogopa. Mwanadamu anaweza kunitenda nini?
12Ee Mungu, nina nadhiri kwako, nitakutolea wewe sadaka zangu za shukrani.
13Kwa kuwa umeniokoa toka kwenye mauti na miguu yangu kwenye kujikwaa, ili niweze kuenenda mbele za Mungu katika nuru ya uzima.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu — CC BY-SA 4.0. Where these translations come from.

Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc. Available free at biblica.com and open.bible. Text unchanged, used under CC BY-SA 4.0.