A shepherd leads sheep beside water, through a ravine, and toward an abundant table

Zaburi 23

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
1Mwenyezi Mungu ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.
2Hunilaza katika malisho ya majani mabichi, kando ya maji matulivu huniongoza,
3hunihuisha nafsi yangu. Huniongoza katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.
4Hata nikipita katikati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya, kwa maana wewe upo pamoja nami; fimbo yako na mkongojo wako vyanifariji.
5Waandaa meza mbele yangu machoni pa adui zangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, kikombe changu kinafurika.
6Hakika wema na upendo vitanifuata siku zote za maisha yangu, nami nitakaa nyumbani mwa Mwenyezi Mungu milele.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu — CC BY-SA 4.0. Where these translations come from.

Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc. Available free at biblica.com and open.bible. Text unchanged, used under CC BY-SA 4.0.