Rebellious rulers gather below a newly anointed king standing securely on Zion

Zaburi 2

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
1Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya, na makabila ya watu kula njama bure?
2Wafalme wa dunia wanajipanga na watawala wanajikusanya dhidi ya Mwenyezi Mungu na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake.
3Wanasema, “Tuvunje minyororo yao na kuvitupilia mbali vifungo vyao.”
4Yeye anayetawala mbinguni hucheka, Bwana huwadharau.
5Kisha huwakemea katika hasira yake na kuwaogopesha katika ghadhabu yake, akisema,
6“Nimemtawaza Mfalme wangu juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.”
7Nitatangaza amri ya Mwenyezi Mungu: Yeye aliniambia, “Wewe ni Mwanangu; leo mimi nimekuwa Baba yako.
8Niombe, nami nitayafanya mataifa kuwa urithi wako, na miisho ya dunia kuwa milki yako.
9Utawapondaponda kwa fimbo ya chuma, na kuwavunjavunja kama chombo cha mfinyanzi.”
10Kwa hiyo, ninyi wafalme, kuweni na hekima; mwonyeke, enyi watawala wa dunia.
11Mtumikieni Mwenyezi Mungu kwa hofu na mshangilie kwa kutetemeka.
12Mbusu Mwana, asije akakasirika nawe ukaangamizwa katika njia yako, kwa maana hasira yake inaweza kuwaka ghafula. Heri wote wanaomkimbilia.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu — CC BY-SA 4.0. Where these translations come from.

Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc. Available free at biblica.com and open.bible. Text unchanged, used under CC BY-SA 4.0.