
Zaburi 137
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
1Kando ya mito ya Babeli tuliketi, tukaomboleza tulipokumbuka Sayuni.
2Kwenye miti ya huko tulitundika vinubi vyetu,
3kwa maana huko hao waliotuteka walitaka tuwaimbie nyimbo; watesi wetu walidai nyimbo za furaha; walisema, “Tuimbieni wimbo mmoja kati ya nyimbo za Sayuni!”
4Tutaimbaje nyimbo za Mwenyezi Mungu, tukiwa nchi ya kigeni?
5Nikikusahau wewe, ee Yerusalemu, basi mkono wangu wa kuume na usahau ujuzi wake.
6Ulimi wangu ushikamane na kaakaa la kinywa changu kama sitakukumbuka wewe, kama nisipokufikiri Yerusalemu kuwa furaha yangu kubwa.
7Kumbuka, Ee Mwenyezi Mungu, walichokifanya Waedomu, siku ile Yerusalemu ilipoanguka. Walisema, “Bomoa, bomoa hata misingi yake!”
8Ee binti Babeli, uliyehukumiwa kuangamizwa, heri yeye atakayekulipiza wewe kwa yale uliyotutenda sisi:
9yeye ambaye atawakamata watoto wako wachanga na kuwaponda juu ya miamba.
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu — CC BY-SA 4.0. Where these translations come from.
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc. Available free at biblica.com and open.bible. Text unchanged, used under CC BY-SA 4.0.