
Zaburi 131
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
1Moyo wangu hauna kiburi, Ee Mwenyezi Mungu, macho yangu hayajivuni; sijishughulishi na mambo makuu kunizidi wala mambo ya ajabu mno kwangu.
2Lakini nimetuliza na kunyamazisha nafsi yangu; kama mtoto aliyeachishwa kunyonya na mama yake, kama mtoto aliyeachishwa kunyonya ndivyo ilivyo nafsi iliyo ndani yangu.
3Ee Israeli, mtumaini Mwenyezi Mungu tangu sasa na hata milele.
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu — CC BY-SA 4.0. Where these translations come from.
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc. Available free at biblica.com and open.bible. Text unchanged, used under CC BY-SA 4.0.