
Zaburi 126
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
1Mwenyezi Mungu alipowarejesha mateka Sayuni, tulikuwa kama watu walioota ndoto.
2Vinywa vyetu vilijaa kicheko, ndimi zetu zilijaa nyimbo za shangwe. Ndipo iliposemwa miongoni mwa mataifa, “Mwenyezi Mungu amewatendea mambo makuu.”
3Mwenyezi Mungu ametutendea mambo makuu, nasi tumejaa furaha.
4Ee Mwenyezi Mungu, turejeshee watu wetu waliotekwa, kama vijito katika Negebu.
5Wapandao kwa machozi watavuna kwa nyimbo za shangwe.
6Yeye azichukuaye mbegu zake kwenda kupanda, huku akilia, atarudi kwa nyimbo za shangwe, akichukua miganda ya mavuno yake.
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu — CC BY-SA 4.0. Where these translations come from.
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc. Available free at biblica.com and open.bible. Text unchanged, used under CC BY-SA 4.0.