A community helps one another escape rushing water as a small bird flies from an opened net

Zaburi 124

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
1Kama Mwenyezi Mungu hangekuwa upande wetu; Israeli na aseme sasa:
2kama Mwenyezi Mungu hangekuwa upande wetu, watu walipotushambulia,
3hasira yao ilipowaka dhidi yetu, wangetumeza tukiwa hai,
4mafuriko yangegharikisha, maji mengi yangetufunika,
5maji yaendayo kasi yangetuchukua.
6Ahimidiwe Mwenyezi Mungu, ambaye hakuruhusu turaruliwe kwa meno yao.
7Tumeponyoka kama ndege kutoka mtego wa mwindaji; mtego umevunjika, nasi tumeokoka.
8Msaada wetu ni katika jina la Mwenyezi Mungu, Muumba wa mbingu na dunia.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu — CC BY-SA 4.0. Where these translations come from.

Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc. Available free at biblica.com and open.bible. Text unchanged, used under CC BY-SA 4.0.