An elder teaches children in a sanctuary courtyard as families distribute food across fertile fields

Zaburi 111

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
1Msifuni Mwenyezi Mungu. Nitamtukuza Mwenyezi Mungu kwa moyo wangu wote, katika baraza la wanyofu na katika kusanyiko.
2Kazi za Mwenyezi Mungu ni kuu, wote wanaopendezwa nazo huzitafakari.
3Kazi zake zimejaa fahari na utukufu, haki yake hudumu daima.
4Amefanya maajabu yake yakumbukwe, Mwenyezi Mungu ni mwenye neema na huruma.
5Huwapa chakula wale wanaomcha, hulikumbuka agano lake milele.
6Amewaonesha watu wake uwezo wa kazi zake, akiwapa nchi za mataifa mengine.
7Kazi za mikono yake ni za uaminifu na haki, mausia yake yote ni ya kuaminika.
8Zinadumu milele na milele, zikifanyika kwa uaminifu na unyofu.
9Aliwapa watu wake ukombozi, aliamuru agano lake milele: jina lake ni takatifu na la kuogopwa.
10Kumcha Mwenyezi Mungu ndicho chanzo cha hekima, wote wanaozifuata amri zake wana busara. Sifa zake zadumu milele.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu — CC BY-SA 4.0. Where these translations come from.

Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc. Available free at biblica.com and open.bible. Text unchanged, used under CC BY-SA 4.0.