Joyful families, musicians, shepherds, and harvest bearers enter Jerusalem's open gates together

Zaburi 100

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
1Mpigieni Mwenyezi Mungu kelele za shangwe, dunia yote.
2Mwabuduni Mwenyezi Mungu kwa furaha; njooni mbele zake kwa nyimbo za shangwe.
3Jueni kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mungu. Yeye ndiye alituumba, sisi tu mali yake; sisi tu watu wake, kondoo wa malisho yake.
4Ingieni malangoni mwake kwa shukrani na katika nyua zake kwa kusifu, mshukuruni yeye na kulisifu jina lake.
5Kwa maana Mwenyezi Mungu ni mwema na fadhili zake zadumu milele; uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu — CC BY-SA 4.0. Where these translations come from.

Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc. Available free at biblica.com and open.bible. Text unchanged, used under CC BY-SA 4.0.