Bildad speaking beneath a vast night sky and dimmed moon

Ayubu 25

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
1Ndipo Bildadi Mshuhi akajibu:
2“Mamlaka na kuheshimiwa ni vyake Mungu; yeye huthibitisha amani katika mbingu juu.
3Je, majeshi yake yaweza kuhesabika? Ni nani asiyeangaziwa na nuru yake?
4Mtu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu? Awezaje mtu aliyezaliwa na mwanamke kuwa safi?
5Ikiwa hata mwezi sio mwangavu nazo nyota si safi machoni pake,
6sembuse mtu ambaye ni funza: mwanadamu ambaye ni buu tu!”

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu — CC BY-SA 4.0. Where these translations come from.

Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc. Available free at biblica.com and open.bible. Text unchanged, used under CC BY-SA 4.0.