Jeremiah reassuring a weary Baruch beside rolled blank scrolls as storm clouds pass over Jerusalem

Yeremia 45

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
1Hili ndilo nabii Yeremia alilomwambia Baruku mwana wa Neria katika mwaka wa nne wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, baada ya Baruku kuandika katika kitabu maneno ambayo yalitoka kinywani mwa Yeremia wakati ule:
2“Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, akuambialo wewe Baruku:
3Ulisema, ‘Ole wangu! Mwenyezi Mungu ameongeza huzuni juu ya maumivu yangu, nimechoka kwa kulia kwa uchungu wala sipati pumziko.’ ”
4Lakini Mwenyezi Mungu akasema, “Mwambie hivi: ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Nitakibomoa kile nilichokijenga, na kung’oa kile nilichokipanda katika nchi yote.
5Je, utajitafutia mambo makubwa kwa ajili yako mwenyewe? Usiyatafute hayo. Kwa kuwa nitaleta maangamizi juu ya watu wote, asema Mwenyezi Mungu, lakini popote utakapoenda, nitayaokoa maisha yako.’ ”

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu — CC BY-SA 4.0. Where these translations come from.

Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc. Available free at biblica.com and open.bible. Text unchanged, used under CC BY-SA 4.0.